Tuesday , 7th Jan , 2020

Zaidi wenyeviti 220 wa mitaa ya halmashauri ya jiji la Dodoma wametishia kuachana na kazi hiyo kutokana na kukosa mihuri ya kufanyia kazi.

Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Jiji la Dodoma

Wamedai kuwa hali hiyo inawasababishia migongano na wananchi wao wanapohitaji huduma za kiserikali.

Baadhi yao wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Patrobas Katambi katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabili, wamesema tangu wachaguliwe hawajapatiwa nyaraka muhimu za ofisi na kuwasababishia uhasama na wananchi waliowachagua.

Kwa upande Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Patrobas Katambi amewataka wenyeviti hao wawe na subira na kuahidi kulifikisha suala hilo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kupata muafaka.

Wenyeviti hao wameingia madarakani kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2019.