Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Yanga yasubiri barua, M/Kiti aikana kamati saa 72

Thursday , 23rd Jan , 2020

Uongozi wa klabu ya Yanga umeendelea kusisitiza kuwa unasubiri barua rasmi ya adhabu iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Ligi kufuatia madai ya utovu wa nidhamu yaliyofanywa na wachezaji wake na kocha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto

Akiongea na EATV/Radio Digital, Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wao hawawezi kulalamikia chochote kwa sasa bali wanasubiri barua rasmi kutoka kamati hiyo.

"Siwezi kuzungumzia hilo, sijalalamika na wala Yanga haijalalamika bali  tumesema tunasubiri taarifa tuisome na tujiridhishe na kanuni walizotumia ndio tujue tunakubali au tunakataa", amesema Bumbuli.

Jumatano, Januari 22, Kamati ya Uendeshaji wa Ligi ilitoa adhabu kwa kuwafungia mechi 3 na faini ya Sh. 500,000 wachezaji Kelvin John na Majaliwa Shaban wa Mbeya City na Mrisho Ngassa, Ramadhani Kabwili na Cleafas Sospeter wa Yanga kwa kosa la kugoma kuingia vyumba vya kubadilishia nguo, huku pia ikitoa onyo kwa kocha wa Yanga, Luc Eymael kutokana na kauli yake kwa mwamuzi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji amesema kuwa kamati hiyo ya maamuzi haiitwi 'kamati ya saa 72' kama inavyoitwa na watu wengi.

"Hii sio Kamati ya saa 72 kama watu wanavyopenda kuiita, hii ni kamati ya uendeshaji wa ligi lakini kuna watu tu na utashi wao walitaka maamuzi yafanyike kwa uharaka zaidi ndio wakaita hivyo", amesema Mguto.
 

HABARI ZAIDI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi