Thursday , 30th Jan , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema ataanzisha msako wa kuwakamata na kuwaweka rumande wazazi wote, ambao hadi sasa bado hawajawapeleka watoto wao kuripoti shuleni kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza na kwamba dhamana ya mzazi atakapokamatwa itakuwa ni mtoto kuanza shule.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

RC Gambo amesema kuwa licha ya Mkoa huo kufaulisha Jumla ya watoto 35,254, lakini taarifa ya Januari 24, 2020, imeonesha kuwa ni wanafunzi 25,483, ambao ni sawa na asilimia 72 ndio wamewasili katika shule walizopangiwa.

"Kuanzia sasa wanafunzi kokote waliko, wazazi kokote waliko, viongozi wangu wote katika ngazi zote, wataanza msako maalumu wa kuwatafuta wazazi wote ambao watoto wao hawajapelekwa shule na tukimkamata mzazi tutamuweka lock up na dhamana yake ni mtoto kuripoti shuleni" amesema RC Gambo.