Wasanii wanaounda kundi la Mabantu kushoto ni Muuh, kulia Twaah
Wakipiga stori na EATV & EA Radio Digital, wasanii hao wamesema wanaonekana kujichubua kwa sababu ya vyakula wanavyokula na kutumia mafuta ya nazi tu.
"Hapana sio kweli sisi hatufanyi hiko kitu, wanasema tunajichubua na unavyoniona mimi hata baba yangu yupo hivihivi ni rangi za ukoo tu na mafuta ninayotumia ni ya nywele kwenye nywele ni nazi tu situmii losheni wala nini" Muuh Mabantu.
Pia kwa upande wa msanii mwenzake Twaah Mabantu ameongeza kusema "Sisi hatujichubui labda vyakula tunavyokula huenda ndiyo vinatufanya tuwe hivi, lakini hatufanyi hayo mambo kabisa".