Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mbeya: Ajiua kwa risasi kwa kushindwa kulipa mkopo

Tuesday , 19th May , 2020

Mfanyabiashara wa madini na mbao, Jonas Mahenge (52) aliyekuwa akiishi Kata ya Uyole Jijini Mbeya, amejiua kwa kujipiga risasi mdomoni na kutokea utosini kwa kutumia bunduki yake baada ya kushindwa kurejesha mkopo wa Tsh milioni 100 aliouomba benki.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema  tukio hilo limetokea Mei 18, 2020 saa tisa usiku, ambapo mfanyabiashara huyo alijipiga risasi kwa kutumia bunduki aina ya Pisto Browning yenye namba za usajili 00099307.

Kufuatia tukio hilo,  Kamanda Matei amewashauri wananchi kuwa na mpango mkakati wakati wa kufanya shughuli za kiuchumi zozote kabla ya kuchukua mkopo wowote na kwamba kabla ya kufanya biashara yoyote wawashirikishe wataalamu wa biashara kwa ushauri ili washauri mapato na matumizi ya biashara zetu.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limemtia nguvuni, Marko Kandonga (78) Mkazi wa Kilambo, Kata ya Njisi wilayani Kyela kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali bila kibali ikiwamo  ngozi moja ya mnyama aina ya Komba, ngozi ya nyoka aina ya chatu  na mkia wa Ngiri ambazo zote thamani yake bado haijapatikana lakini ufuatiliaji unaendelea.

HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini

Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari