
Mwanaume aliyefumaniwa akiwa kituo cha polisi
Imeelezwa kuwa mume wa mwanamke huyo ambaye ni Mwanajeshi alirudi ghafla nyumbani bila taarifa na kumkuta mkewe na mwanaume huyo wakiwa ndani, ndipo alipofanikiwa kukimbia.
Alifika kituoni akiwa mwenye wasiwasi mkubwa huku akiomba msaada wa kuokolewa dhidi ya mume wa mwanamke aliyekutwa naye, ambaye alikuwa anamtafuta kila mahali.
Akiandikisha taarifa katika kituo cha polisi, mwanaume huyo aliyefumaniwa amesema kuwa mwanamke alimuambia kuwa ni mjane, baada ya mumewe kufariki katika shambulio la Dusit d2 mwaka uliopita.