Msanii na Mwanasiasa Prof Jay
Akitoa funzo hilo kupitia post aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram na Twitter Prof Jay ameandika kuwa, "Nimejifunza kwamba sisi wanadamu inatupasa kuchunga sana ndimi zetu, kutafakari kwa kina kauli zetu na inapobidi ni kufunga kabisa mabakuli yetu kwani malipo yapo hapa hapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibu" kutoka kwa Prof Jay.
Tayari Prof Jay ametangaza nia ya kugombania tena kwa miaka mitano ijayo ya kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Mikumi, Mkoani Morogoro.