Thursday , 23rd Jul , 2020

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara TPLB imefungua mchakako wa ukusanyaji maoni kuhusu maboresho ya kanuni za ligi msimu ujao wa 2020-21.

Afisa Mtendaji mkuu wa TPLB, Almas Kasongo akizungumza na Waandishi wa Habari.

Taarifa ya bodi ya ligi inasema mnamo Julai 11 iliwaandikia watendaji wakuu wa klabu zote za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na daraja la pili kuwapa taarifa juu ya mchakato huo.

TPLB inawaomba wadau wa soka wakiweo wanahabari, vyama vya soka vya Mikoa na Wilaya, vyama shirki (FRAT, TAFCA, TASMA, & SPUTANZA) pamoja na wadau wengine kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

Mwisho wa kupokea maoni hayo ya maboresho ya kanuni za ligi kwa msimu ujao ni julai 31 na maoni hayo yawasilishwe bodi ya ligi kuu.

Taarifa hii inafuatia baada ya siku chache zilizopita wadau mbalimbali wa soka kulalamikia juu ya kanuni za uendeshaji wa ligi hapa nchini kuwa na mapungufu hasa mabadiliko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakifanyoika. na muda mwingine hata vilabu vimeonekana kutojua baadhi ya kanunu za ligi wanazoshiriki.