Thursday , 6th Aug , 2020

Klabu ya soka ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekua mlinzi wa Coastal Union ya Tanga, Ibrahim Mohamed ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Beki Ibrahim Mohamed (Pichani) akisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Simba.

Nyota huyo alitengeneza safu bora ya ulinzi ya Timu ya Coastal Union ya Mkoani Tanga akiwa na Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye ametimkia kwa watani wa jadi wa timu ya Simba, Dar Young Africans yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani Jijini Dar es salaam.

Ilielezwa kuwa Ame alikua akiwindwa na Yanga ambao walikua na nia ya kutengeneza safu bora ya ulinzi kama nyota hao walivyokua katika klabu ya Coastal Union lakini mpango huo ukaingiliwa na wekundu wa msimbazi .

Ame anatarajiwa kwenda kutengeneza safu bora ya ulinzi kwa siku za usoni na Kennedy Juma ambaye ameanza kuonyesha ukomavu katika klabu hiyo bingwa mara tatu mfululizo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

KWA NINI USAJILI HUU?

Ikumbukwe safu ya ulinzi ya timu ya Simba, inawachezaji wenye umri mkubwa wakiwemo Erasto Nyoni, Pascal Serge Wawa ambao hawana muda mrefu wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya soka nchini.