Mmiliki wa timu ya Newcastle Mike Ashley (Pichani) akitafakari jambo.
Mike Ashley ambaye ndiyo Mmilikiwa timu hiyo mwishoni mwa mwaka 2017 alitangaza kuiweka sokoni timu yake ilikupata mmiliki mwingine bila mafanikio hadi mwaka 2020 alipojitokeza Mfanyabiashara Prince Mohamed bin Salmin kutoka Saudi Arabia aliyekusudia kuichukua klabu hiyo.
Baada ya kushindikana.Mwana wa mfalme Bin Salmin alikata tamaa hadi ilipojitokeza kampuni nyingine Bellagraph Nova Group (BNG) ya Singapore ambayo haijaripotiwa kuwa na kashfa ambazo zilikua kikwazo wa ununuzi wa awali kufanyika.
Kama mpango huu utafanikiwa basi huwenda ukaongeza ushindani mkubwa kwenye ligi ya ya England kama ilivyokuwa kwa Chelsea na Manchester City kufanya mapinduzi makubwa ya kiushindani baada ya kununuliwa na Matajiri wa Mataifa mengine.






