P Funk Majani kulia, kushoto ni Marehemu mama yake Aunt Sheilah
Mipango ya Mazishi inaendelea kufanywa, kwa sasa Msiba upo Kilosa mkoani Morogoro na ndipo atazikiwa huko kwa sasa mipango ya kurudisha mwili wa Mama P Funk Majani inaratibiwa.
Akizungumza EATV & EA Radio Digital, Kaka wa Marehemu Fadhili Kiholi amesema "Mpaka sasa hivi mwili bado upo Uholanzi pia tunafanya michakato ya mwili kurejea hapa nchini, tutaondoka leo jioni na taratibu zote tunatarajia kuzifanya wiki ijayo, Marehemu alikuwa akiishi Tanzania na alienda Uholanzia mwezi wa 9 mwaka jana kama sehemu ya matibabu, huwa anaendaga mara kwa mara Uholanzi ila muda huu amekaa kidogo, pia mipango ya mazishi itafanyika Kilosa Morogoro kwenye ardhi aliyozaliwa".