Monday , 12th Oct , 2020

Kocha wa klabu ya Barcelona, Ronald Koeman amesema kuwa Luis Suarez angeweza kukaa Barcelona kumthibitishia kuwa amekosea badala ya kuhamia Atletico Madrid.

Kocha wa Barcelona, Ronald Koeman akiwa mazoezini na kikosi chake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliambiwa hahitajiki tena msimu huu wa joto baada ya kampeni duni ya 2019-20 na alijiunga zake na Atletico Madrid kwa pauni milioni 5 baada ya uwezekano wa kuhamia Juventus kuvunjika.

"Kwa Suarez, ilikuwa ngumu sana kwake kuanza kucheza na nikamjulisha hilo. Aliona ni ngumu, lakini sikuwahi kuwa na shida naye kabisa, "Koeman alisema.

"Alifanya mazoezi kama kawaida, vizuri. Hatimaye alifanya uchaguzi wa kuondoka na nikasema ikiwa hautaondoka, kwa sababu yoyote, basi wewe ni mmoja katika kikosi changu, basi unaweza kuthibitisha kuwa nilikuwa nimekosea".

Kocha huyo pia, amefunguka na kusema kuwa, alimfuata Messi na kumwambia"Najua umekata tamaa na unadhani ni aibu kubwa kwa kuwa Suarez anaondoka lakini hayo ni maamuzi ya klabu".

Suarez alikuwa na mafanikio ya miaka sita huko Nou Camp, akishinda ligi ya mabingwa na mataji manne ya La Liga, na ameanza vyema katika klabu yake mpya akifumania nyavu mara mbili.