Msanii Killy kushoto na Alikiba wakati alipokuwa Kings Music
Killy amesema hivyo mbele ya waandishi wa habari baada ya kujibu tetesi ambazo zinadai kuwa amefuta namba za wasanii wa Kings Music Records na hawana mawasiliano tena baada ya kusainiwa Konde Gang ya Harmonize.
"Hizi ni harakati na maamuzi pia ni muendelezo wa maisha ya muziki, Konde Gang wamenipokea kwa mikoni miwili, kuna upendo sana na tunaishi kifamilia kabla ya kazi, sijafuta namba ya mtu yeyote kila kitu kipo vilevile wale bado ni ndugu zangu na hatujagombana sijaongea na Alikiba ila Abdukiba nazungumza naye" amesema Killy
Killy na Cheed walitangaza kujitoa Kings Music Records ya Alikiba siku ya Aprili 14, 2020 ambapo kwa sasa wapo lebo ya Konde Gang chini ya msanii Harmonize.