Saturday , 24th Oct , 2020

Uongozi wa Maafande wa Ruvu Shooting umejinasibu kutia chumvi kwenye kidonda kibichi kwa kuifunga Simba katika mchezo wa ligi utakaopigwa uwanja wa Uhuru siku ya Jumatatu saa 10 jioni.

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire akiwa katika studio za East Africa Radio.

Afisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire amesema katika mchezo wao wa Jumatatu wamepanga kuwafunga Wekundu hao tena kwa kuonyesha soka safi ambalo amelipa jina la pira la kaukau.

"Hawachezi mpira unaojulikana kama pira biriani, kama Prisons waliwafunga vile, sisi wanajeshi wenyewe je itakuwaje"amesema Masau Bwire.

Masau ameongeza kuwa baada Prisons kuwafunga wao Jumatatu watawapapasa na kuwakung'uta ambayo ndio staili yao mpya ya msimu huu.

Mabingwa hao watetezi mara tatu mfululizo walikubali kipigo cha bao moja kutoka kwa Maafande wengine wa Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga