Wednesday , 28th Oct , 2020

Bingwa wa dunia wa mita 100 katika riadha, Christian Coleman amepigwa marufuku kwa miaka miwili kushiriki mashindano mbalimbali baada ya kukosa kufeli vipimo vya dawa za kuongeza nguvu mara tatu.

Mwanariadha, Christian Coleman akiwa katika moja ya mashindano yake aliyoshiriki.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amesimamishwa kazi kutoka 14 Mei 2020, atakosa michuano ya Olimpiki ya Tokyo iliyoahirishwa hadi mwaka ujao.

Coleman alishinda medali ya dhahabu ya mita 100 kwenye Mashindano ya Dunia huko Doha mnamo 2019.

Mwakilishi Emanuel Hudson alithibitisha kwamba mmiliki wa rekodi ya ulimwengu wa mita 60 atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kitengo cha Uadilifu (AIU) kwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas).

Hudson alielezea uamuzi huo kama "bahati mbaya", na kuongeza: "Bwana Coleman hana la kusema zaidi hadi wakati ambapo kesi hiyo inaweza kusikilizwa katika mahakama yenye mamlaka."

Bingwa mara mbili wa ulimwengu Coleman, ambaye pia alishinda medali ya dhahabu mbio za mita 400 huko Doha, ana siku 30 kuwasilisha rufaa. Alisimamishwa kwa muda mnamo Juni baada ya kukosa mtihani wa tatu mnamo Desemba 2019.