
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Salum Hamduni.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 9, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, hii ni baada ya taarifa kusambaa kwamba Lema anashikiliwa nchini Kenya, baada ya kuingia bila kuwa na nyaraka muhimu.
"Usalama wake hauko hatarini, yuko sawasawa tu na hakuna tishio lolote dhidi ya maisha yake", amesema Kamanda Hamduni.
Imeelezwa kuwa jana Novemba 9, 2020, Lema alishindwa kutoa nyaraka hizo muhimu kwa madai ya kuwa alikuwa anahofia maisha yake na kwamba alikuwa anaelekea nchini Kenya kwa ajili ya kutafuta hifadhi.