Wednesday , 18th Nov , 2020

Wamiliki wa viwanda vya kukamua na kusindika alizeti, mkoani Manyara, wanakabiliwa na uhaba wa malighafi kutokana na kupanda kwa bei ya zao hilo kutoka shilingi elfu thelathini (30,000) hadi elfu sitini (60,000) kwa debe.

Zao la Alizeti

Wakizungumza  na EATV wamiliki hao wa viwanda wameelezea athari za uhaba wa malighafi katika viwanda na jinsi watumiaji  na wafanyabiashara wa mafuta wanavyoteseka kupata mafuta kwa wingi na kwa wakati.

Aidha wasimamizi hao wa viwanda, wameiomba serikali  iwawezeshe wakulima ili waweze kulima kwa wingi alizeti, jambo ambalo litasaidia malighafi ipatikane kwa wingi na changamoto kama hizo zisiendelee kujitokeza.