Monday , 28th Dec , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Bw. Revocatus Kuuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Bw. Kuuli hii leo akiwa ziarani Mkoani humo, ambapo ametaja sababu za kutengua uteuzi huo kuwa ni kutokana na kiongozi huyo  kukabiliwa na tuhuma za kujitwalia ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.

Suala la Mkurugenzi wa hapa ninalifahamu na kuna wakati nilimtuma mkuu wa mkoa kuja kushughulikia ishu zake, kwa sababu bado hajajirekebisha namsimamisha kazi kuanzia leo huko aliko apelekewe barua kuwa hana kazi”, amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Tabora Dkt. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja, wakati akiwa anajiandaa kumteua Mkurugenzi mwingine.