Monday , 4th Jan , 2021

Mabingwa watetezi wa EPL Klabu ya Liverpool saa 5:00 kamili usiku wa leo tarehe 4 Januari 2021 inarataji kushuka dimbani ugenini kuchuana na watakatifu wa Maria, klabu ya Southampton kwenye mchezo wa mzunguko wa 17 wa ligi Kuu England.

Kikosi cha Mabingwa watetzi wa EPL, Liverpool.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Kocha wa SOTON, Ralph Hassenhult amerejea baada ya kumaliza siku 10 za kujitenga kufuatia mke wake kukutwa na COVID-19. 

Wakati kocha huyo anarejea kikosini, wachezaji Jannik Vestergaard na Nathan Redmond watakosekana kutokana na majeraha waliyoyapata.

Kwa upande wa Liverpool, wanatazamiwa kujumuika kikosini na kiungo wake Thiago Alcantara aliyepona majeraha yake ya goti baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili pamoja na winga wake Xhedran Shaqiri ilhali Nats Williams akiendelea kuchukua nafasi ya Joel Matip.

Liverpool ambaye anasare mbili mfululuzizo, anaingia kwenye mchezo huo akiwa bado kinara kwenye msimamo EPL akiwa na alama 33 sawa na Manchester United anayeshika wapili jambo linalofanya Liverpool kuingia na mahesabu makali ya kutaka kupata alama 3 ili kumkimbia Manchester United.

Southampton kwasasa inashika nafasi ya 9 wakiwa na alama 26 na kama wakifanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo watafikisha alama 29 basi watapanda hadi nafasi ya 6 na kuwashusha Everton kwa utofauti wa magoli.

Liverpool haijapoteza mchezo kati ya nane ya mwisho waliyocheza dhidi ya Southampton, wakishinda 6 na kutoa sare michezo 2 wakati watakatifu wameweka rekodi ya ushindi kwenye michezo 10 aliyocheza EPL na bingwa mtetezi akiwafunga Man Utd, Arsenal, Blackburn, Chelsea, Man City na Leicester City.