
Mhamasishaji Joel Nanauka
Kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio huyu hapa ni mhamasishaji Jole Nanauka, anafafanua sababu za watu kushindwa kufanikisha malengo yao wanaojiwekea mwanzoni mwa mwaka hasa kwa vijana.
"Watu wengi wanakuwa na malengo mengi kila mwanzo wa mwaka ila mwisho wa siku hawakamilishi chochote, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Scranton Marekani kinasema ni 8% tu ya malengo yanayofanikiwa kila mwisho wa mwaka na 92% huwa yanafeli na 25% huwa wanaachana na malengo yao baada ya wiki ya kwanza"
"Sababu zinazofanya watu kutofanikisha malengo yao hasa vijana ni kukosa vipaombele, yaani kuwa na malengo mengi kuliko uwezo wao wa kutimiza, kikawaida kunatakiwa maeneo 6 ili kutimiza malengo yako kama afya, fedha, taaluma, ujuzi, mahusiano na biashara" ameongeza
Bonyeza hapa kwenye video kutazama interview ya Hamis akimlilia Harmonize