
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi, Almas Kasongo.
(Barua ya wazi ya Bodi ya Ligi inayotoa taarifa ya michezo ya viporo na ile ya mzunguko wa 19 wa VPL.)
Klabu ya Simba na Namungo ndivyo vilabu viwili pekee kwenye uwakilkishi wa Tanzania kwenye michuano ya Afrika ambavyo ndivyo vinavyotarajiwa kuanza kucheza michezo yake ya viporo wakati wanachuana kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Afrika.
Simba wanaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo wametinga makundi wakiwa kundi A na bingwa mtetezi na bingwa wa kihistoria ya michuano hiyo, klabu ya Al Ahly ya Misri, El Merick ya Sudan na AS Vita ya DR Congo.
Namungo watacheza mchezo wa mtoano wa mwisho kutafuta historia ya kutinga kwa mara ya kwanza kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika endapo wakifanikiwa kuitoa Primiero de Agosto ya Angola tarehe 12 Februari.