Monday , 25th Jan , 2021

Klabu ya Chelsea imemfuta kazi aliyekuwa kocha wake Frank Lampard kufuatia matokeo mabaya klabuni hapo hususani kwenye EPL kwa kupoteza michezo mitano, sare mbili na kupata ushindi kwenye michezo miwili pekee katika michezo kumi ya mwisho.

Aliyekuwa kocha wa Chelsea, Frank Lampard.

Uamuzi wa kumtimua kazi Lampard ambaye amedumu kwa miezi 18 umethibitishwa na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovic ambaye amesema haukuwa uamuzi mrahisi kuufikia kutokana na urafiki wa karibu pamoja na heshima ya Lampard klabuni hapo.

Lampard alitangazwa kuifundisha Chelsea 4 Julai 2019 na kusaini kandarasi ya miaka 3 na kuwa kocha muingereza wa kwanza kuifundisha Chelsea baada ya takribani miaka 20 na kufanikiwa kumaliza kwenye nafasi 4 za juu pamoja na kucheza fainali ya FA.

Mbadala anayetajwa kuchukua mikoba ya Frank Lampard ni kocha Thomas Tuchel aliyekuwa kocha wa klabu ya PSG na kuwaongoza matajiri hao wa jiji la Paris kutwaa mataji mawili ya ligi kuu nchini Ufaransa na kucheza fainali ya klabu bingwa ulaya.