Friday , 29th Jan , 2021

Kocha wa Klabu ya PSG, Mouricio Pochetino ameweka wazi kwamba anaimani kubwa kuwa mshambuliaji wake Kylian Mbappe ataendelea kusalia klabuni hapo licha ya tetesi za kuhiatajiwa na matajiri wa Real Madrid ya Hispania.

Mouricio Pochetino (kushoto) na Kylian Mbappe (kulia) wote kwa pamoja ni watumishi wa klabu ya PSG ya Ufaransa.

Pochetino ambaye amejiunga na PSG majuma kadhaa yaliyopita, amesema ni kweli amesikia kuhitajiwa kwa nyota wake na Los Blancos, lakini Mbappe yupo kwenye mipango ya muda mrefu na kikosi chake hivyo jitihada za kumbakisha zitaendelea kufanyika.

Mbape mwenye umri wa miaka 22, amebakisha miezi 18 katika mkataba wake ambao unatarajiwa kutamatika mwakani, anatajwa kutaka kuondoka PSG na Real Madrid ikitajwa ndiyo klabu inayopewa kipaumbele kuinasa saini ya mfaransa huyo.

Katika msimu huu, Mbappe amecheza mechi takribani 17 za mashindano yote, amefunga mabao 14 na kutoa pasi sita zilizozalisha mabao akiwa na PSG.