IGP Simon Sirro
IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya kikao kazi na Polisi Wasaidizi waliopo Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa, weledi, ufanisi na kujituma kutasaidia kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii wanayoihudumia.
Sambamba na hayo lakini amesisitiza suala la nidhamu, wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku katika kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu.
Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, uwepo wa Polisi Wasaidizi umesaidia kuwezesha mamlaka na Halmashauri mbalimbali zilizopo nchini kuendelea kuimarika.









