Elizabeth Michael na Majizzo wakiwa wanafunga ndoa leo
Kupitia picha ambazo zimepostiwa mitandaoni zimeonesha wawili hao wakila kiapo cha kufunga ndoa hiyo ambayo imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Gasper, Mbezi Beach Jijini Dar es Saalm.
Mahusiano ya Elizabeth Michael Lulu na Majizzo ni ya muda mrefu na walikuwa wote kwenye kipindi ambacho Lulu alikuwa na kesi ya kuua bila kukusudia na kufikia Septemba 30, 2018 Majizzo alimvalisha pete ya uchumba Lulu.