
Mbunge wa Jimbo la Muheza Tanga na msanii Mwana Fa
Wimbo huo ambao amemshirikisha Vanessa Mdee ulitoka mwaka 2016, sasa kupitia mtandao wa Twitter shabiki yake mmoja ali-post baadhi ya mistari inayopatikana kwenye wimbo huo kwa kuandika.
"Nihonge nanunua nini, kwanini yani? kuna kipi nisichokijua au ina TV ndani"
Baada ya muda mfupi Mwana Fa akajibu post hiyo kwa kuandika "Nilikuwa mdogo na mjeuri, mnisamehe".
Kupitia mtandao wa YouTube, video ya wimbo huo kwa sasa una watazamaji zaidi ya Milioni 5.