Thursday , 18th Mar , 2021

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa pole kwa watanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametoa salamu za pole kwa taifa la Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo Behgjet Pacolli ametoa salamu kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 majira ya saa 12:00 Jioni.

Mama Samia amesema Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.