Thursday , 18th Mar , 2021

Kupitia EATV & EA Radio Digital, msanii wa HipHop na Mwanaharakati Kala Jeremiah aliwahi kusema ni ngumu kumpata Kiongozi kama Rais Dkt John Pombe Magufuli endapo kama ataaondoka madarakani.

Dkt John Pombe Magufuli, kushoto ni msanii Kala Jeremiah

"Rais wa sasa amefanya vitu vingi, mimi naona Rais Magufuli atakapoondoka kwenye uongozi kuna changamoto kubwa ya kumpata mtu mwenye kariba yake kwa sababu kuna miradi mingi na mikubwa ameianzisha, tunahitaji Rais wa dizaini kama yake ujue kuwa kiongozi ni maono kwamba watu wanashida na unatakiwa uwasaidie kama ambavyo amefanya yeye" ameeleza Kala Jeremiah

Taarifa za kifo cha Rais John Pombe Magufuli zimetangazwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu, EATV & EA Radio Digital inatoa pole kwa Taifa zima kwa ujumla kufuatia kwa msiba huu mzito.

Zaidi mtazame hapa Kala Jeremiah akizungumzia hilo.