Thursday , 15th Apr , 2021

Mwenyekiti wa klabu ya Simba kutoka upande wa wanachama Murtaza Mangungu, amewataka mashabiki wao kutokuwa na hofu yeyote katika suala la FCC kwa kuwa wanalifuatilia kwa ukaribu.

Kikosi cha Simba kinachofanya vizuri kwa sasa licha ya mchakato wake wa mabadiliko kutokukamilika

''Ni kweli taarifa hiyo imeleta taharuki kwa mashabiki wa timu yetu,lakini kwa kuwa ni mchakato wa kisheria tunasubiri muongozo wa FCC,nimemsikia mtendaji wa taasisi hiyo akiuzungumzia suala hilo sisi kama Simba tutawapa ushirikiano wowote watakao uhitaji '' alisema Mwenyekiti huyo

Majuzi iliibuka hali ya sintofahamu baada ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi upande wa muwekezaji Mohamed Dewji kuandika kwenye mitandao yake ya kijamii kuhusu kinachoendelea katika tume ya ushindani (FCC)

Ujumbe uliotafsiriwa na wadau wa soka kwamba zoezi la mabadiliko limeshindikana hivyo wanapaswa kuanza upya kwenye hatua za mwanzo kabisa,

Simba ambayo imeanza mchakato wa uwekezaji 2017 bado haijafanikiwa kukamilisha hatua zote muhimu ili muwekezaji waweze kuweka bilioni 20, kwa sasa amekuwa akitoa ruzuku ya bilioni 3 kwa mwaka na kuchagiza mafanikio makubwa ikiwemo ubingwa wa ligi misimu 3 mfululizo,na ushiriki mzuri ligi ya mabingwa Africa ambapo kwa sasa wapo hatua ya robo finali