Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mkurugenzi wa Fedha UDART atimuliwa

Monday , 19th Apr , 2021

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa amemtumbua Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka nchini (UDART) Bi. Suzana Chaula huku akiweka wazi kuwa tatizo lililopo kwenye miradi wa UDART si uwezo bali ni usimamzi mbovu.

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa (kushoto) akiwa kwenye ziara

Mh. Majaliwa amefikia uamuzi huo leo katika ziara yake alioifanya katika kituo cha UDART na kubaini utendaji kazi na ufuatiliaji mbovu katika ofisi hizo uliopelekea uwepo wa mabasi mabovu, mifumo ya kielektroniki na mrundikano wa tiketi katika vituo.

"Tunataka tujenge mradi awamu ya tatu kwenda Gongo la Mboto, tunajenga awamu hii kukusanya fedha kununua mabasi kwa ajili ya awamu nyingine uwezo huo upo, tatizo ni usimamizi hatuwezi kuvumilia msimamizi ambaye hawezi akiwemo na mkurugenzi wa fedha, hatuwezi vumilia utaratibu huu, hii fedha sisi tumekopa World Bank na tunalipa fedha yetu ya ndani ya walipa kodi wa Tanzania, leo tunaweka watu hawafanyi kazi vizuri," amesema Mh. Majaliwa.

Awali Waziri Mkuu ameeleza uwepo wa Mkurugenzi Mkuu UDART kwa miaka mitano katika mradi huo bila kuleta maendeleo yeyote ikiwemo ununuzi wa mabasi mapya huku baadhi ya watendaji wakifumbia macho ubadhirifu unaofanyika.

"Mtu anauza tiketi zake ndipoo auze za serikali na watendaji wapo, wanaona na hawachukui hatua, leo nimewauliza tangu Mkurugenzi Mkuu ameingia UDART ana miaka mitano amenunua mabasi mangapi?, hakuna hata moja anasema hana fedha," amesema Mh. Majaliwa.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi