Monday , 26th Apr , 2021

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Mwita Waitara amempa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Eric Benedict Hamisi siku 14 kuaanda ripoti ya utekelezaji mradi upanuzi bandari ya Tanga na kuikabidhi kwake.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara.

Katika taarifa hiyo,ametaka ufafanuzi  wa namna ya ushindanishwaji wa zabuni, kufuatwa kwa kanuni, kufuatwa kwa ushauri wa kitaalam na nani alihusika katika kutangaza zabuni ya upanuzi huo pia alishangazwa na mkuu wa Mkoa wa Tanga kutokuwa na taarifa za kiasi cha fedha upanuzi wa bandari ya Tanga.

Naibu Waziri Waitara ametoa agizo hilo wakati  alipotembelea bandari ya Tanga kukagua maendeleo ya upanuzi wa bandari hiyo gati namba moja na namba mbili baada ya kunusa dalili za ufisadi.
Kuhusu ubadhirifu katika Mamlaka hiyo,amemuagiza kuwachukukulia hatua za haraka watendaji wote wa mamlaka hiyo kuanzia bahari kuu hadi bandari za maziwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA,Eric Hamisi amesema ameyapokea maelekezo na kuahidi kuyafanyia kazi na kuahidi kuuandaa taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Naibu Waziri kwa muda waliopewa.
Amesema kuwa serikali katika upanuzi wa bandari ya Tanga imwekeza kiasi cha Sh bilioni 500 ambapo katika fedha hizo ni upanuzi wa gati bilioni 256 na uchimbaji wa kina bilioni 172.