
Wacheza mchezo wa mpira wa pete wakiwania mpira.
Rais wa shirikisho hilo, Liz Nicholl amesema, "Australia wamekuja na mpango kazi mzuri na tunaimani wataandaa na kusimamia vizuri sana michuano hiyo kwenye jiji la Sydney kama ambavyo inakuwa mizuri ikifanyika nchini humo”.
“Mchezo wetu unaendelea kukua na kuenea kwa kiwango kikubwa Duniani, tunaangalia mbele kufanya kazi vizuri na chama cha mpira wa pete nchini Australia na tunataraji kupitia mashindano hayo tutatengeneza ujirani mwema kwenye maeneop mengi Duniani”.
Hii ni mara ya tatu kwa nchi ya Australia kuandaa michuano hiyo mikubwa duniani kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete, kwani mwaka 1991 na 2015 walipoandaa michuano hiyo, timu ya taifa ya Australia ya mpira wa pete ilifanikiwa kutwaa ubingwa kwenye ardhi yake ya nyumbani.