Monday , 26th Apr , 2021

Ni 'headilines' za msanii wa filamu na muziki Official Agness ambaye amefunguka chanzo cha kutaka mahari ya Milioni 500 kwa mtu anayetaka kumuoa kwa kusema mahari hiyo ni kujipa thamani kama mwanamke, gharama walizotumia wazazi wake kumlea na kumsomesha.

Msanii Official Agness

Akizungumza kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio wakati anatoa mchanganuo wa mahari hiyo Official Agness ameeleza kuwa 

"Bila milioni 500 hakuna ndoa, kuna gharama nyingi zimetumika kwa wazazi wangu kama shule, chuo hata mimi nimetumia gharama nyingi kufika hapa pia ni mpambanaji pia, akitokea mtu akanilipia Milioni 500 atakuwa ananipenda sana” 

"Nimeamua kujipa thamani wazazi wangu wamepambana sana, kwahiyo siwezi kuolewa kwa gharama ndogo ya Milioni 2 au Milioni  3" amesema Official Agness

Aidha ameendelea kusema wazee wa zamani walidumu kwenye ndoa kwa sababu pesa haikuwa na thamani kwao lakini sasa hivi pesa ndiyo kila kitu kwenye ndoa.