
Guardiola ameshinda mataji 9 tangu ajiunge na Manchester City mwaka 2016
Kauli ya Neville inafuatia baada ya Pep Guardiola kukiongoza kikosi cha Manchester City kutwaa ubingwa wa kombe la Ligi Carabao Cup baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham kwenye mchezo wa fainali, ikiwa ni kwa msimu wa nne mfululizo wanashinda taji hilo chini ya kocha huyo.
‘’Nadhani Man City inaweza kuwa na kocha bora wa muda wote tutaangalia nyuma miaka 10, 15, 20… jinsi tu alivyefanya kazi kwenye nchi tofauti, kutawala mpira sidhani kama nimewahi kuona. Unaangalia jinsi alishinda katika nchi tatu tofauti, sasa anatawala katika nchi hii, atashinda taji la Ligi Kuu wiki chache zijazo, hiyo ni mara ya tatu katika miaka mitano haya ni mafanikio makubwa.” Amesema Gary Niville
Manchester City wapo kwenye nafasi ya kushinda mataji mawili zaidi msimu huu, kwani wanahitaji kushinda michezo miwili inayofata ya Ligi Kuu ili kutwaa ubingwa wa EPL msimu huu. Lakini pia kikosi hicho bado kipo kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya na watacheza dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali utakaochezwa siku ya Jumatano Aprili 28.
Pep alijiunga na Manchester City mwaka 2016, na mpaka sasa amekiongoza kikosi hicho kwenye michezo 286, na ameshinda jumla ya mataji tisa (9) akiwa na timu hiyo kutoka Jiji la Manchester.