
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Bernard Morrison akiwa mazoezini.
Baada ya Morrison kufanya tukio hilo alioneshwa kadi ya njano lakini kamati ya Uendeshwaji na Usimamizi wa Ligi kuu Tanzania bara kupitia kikao chake cha tarehe 27 Aprili 2021, kilipitia ripoti ya mwamuzi wa mchezo huo na tukio lenyewe na kuamua kutotoa adhabu nyingine zaidi.
Uamuzi wa kamati hiyo umetolewa usiku wa kuamkia leo Aprili 29, 2021 na kusomeka kuwa,
“Kamati imejiridhisha na kukubaliana na maelezi yaliyo kwenye ripoti ya mwamuzi wa mchezo tajwa hapo juu kuwa mchezaji wa Simba SC, Bernard Morrison alistahili adhabu ya kadi ya manjano aliyooneshwa kufuatia kitendo cha alichokifanya kisicho cha kiuana michezo cha kumvuta".
Kamati pia imempa onyo kali mchezaji Bernard Morriso kutorudia vitendo vya aina hiyo mchezoni.