
Kylian Mbappe
Nyota huyo wa kifaransa aligusa mpira mara chache sana kuliko golikipa wa Manchester City Ederson.
Mbappe amepewa alama hizo na Jarida la Ufaransa L'Equipe baada ya Paris Saint-Germain kupokea kichapo kwenye mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya dhidi ya Manchester City.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye alikuwa nyota wa mchezo katika raundi iliyopita dhidi ya Bayern Munich, alishindwa kupiga hata shuti moja kwenye lango dhidi ya City huko Parc des Princes.
Licha ya kuwa Mbappe alishapona jeraha lake na kuweza kucheza, lakini hakuweza kufanya chohcote mbele ya John Stones na Ruben Dias kitendo ambacho wengine wametafsiri kama alikua anacheza kwa kujihami sana kitu kilicho sababisha kuonekana hakuwa na mchango wowote uwanjani.