Akina Baba wadaiwa kuwaambukiza Ukimwi mabinti

Wednesday , 12th May , 2021

Mbunge wa Viti Maalum Fatma Toufiq, amedai kuwa akina Baba siku hizi hawawafuati tena wanawake watu wazima ili kuanzisha nao mahusiano badala yake wamekuwa wakiwambilia watoto wadogo hali inayopelekea kuwaambukiza Ukimwi na kupelekea maambukizi mapya kwa watoto wa kike kuwa makubwa.

Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Toufiq

Kauli hiyo ameito hii leo Mei 12, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akichangia hoja ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa hii leo na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima.

"Kundi kubwa ambalo linaonesha lipo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa Ukimwi ni watoto wenye umri wa miaka 14-24, na katika wale vijana 10 wanaoopimwa watoto wa kike 8 ndiyo wanaombukizwa sana, nilikuwa nashauri akina Baba ebu muwaonee huruma hawa watoto, sababu mmeacha kuwafuata akina mama watu wazima mnawafuata hawa watoto", amesema Mbunge Fatma

Aidha ameongeza kuwa "Hebu waacheni hawa watoto wasome watimize malengo yao, haya mambukizi mapya hawa watoto wanayapata kwa akina Baba ambao hawajapima".