Mbunge wa viti maalum Mariam Kisangi
Kauli hiyo ameitoa leo Juni 24, 2021, Bungeni Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu, swali ambalo lilielekezwa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kujibiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo David Silinde.
"Je serikali ina mpango gani wa kuanzisha wilaya mpya ya Ukonga katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kwa kuwa mchakato wa kuanzisha wilaya ya Ukonga ulifanywa 2015 sambamba na uanzishwaji wa Wilaya ya Kigamboni na Ubungo ambazo wakati huo mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na Halmashauri tatu, na wilaya hizo zote zilifanya mchakato wa kuongeza Halmashauri," aliuliza mbunge huyo.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde alisema "Kama kuna nia ya kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Ukonga, anzeni upya mchakato mfuate taratibu zote za kisheria, mlete maombi na sisi tutayapeleka kwa Mhe.Rais na yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ya kuanzishwa wilaya mpya ama kusitisha kwa kadri atakavyoona inafaa".





