
Picha ya Wagosi wa kaya kulia ni Dkt John kushoto ni Mkoloni
Mkoloni amesema endapo Wagosi wa kaya wakiacha muziki itakuwa wamekataa muunganiko wao na jamii kitu ambacho hakiwezekani hivyo wataendelea kufanya mziki.
"Ni muda mrefu tumekaa nje ya game lakini Wagosi wa Kaya hatuwezi kuacha muziki kwa sababu umetuunganisha na jamii ina maana tukiacha itakuwa tunakataa muunganiko wetu na jamii kitu ambacho hakiwezekani" amesema Mkoloni
Wakali hao wameshatoa ngoma kali zilizofanya vizuri kama wauguzi, traffic huyo, gahawa, walimu tuna hali ngumu na bao.