Thursday , 12th Aug , 2021

Spika wa Bunge Job Ndugai, ametoa kauli kuwa subira yavuta kheri hivyo tuendelee kungoja huenda zipo hatua zitakazochukuliwa na Bunge hilo kwa wabunge ambao wametoa kauli zao hadharani kwamba hawapo tayari kuchoma chanjo ya corona.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 12, 2021, alipowasiliana na East Africa Radio na EATV Digital, alipoulizwa swali kuhusu hatua zitazochukuliwa kwa wabunge hao akiwemo Hamphrey Polepole na Askofu Gwajima waliotoa kauli hizo, kwa kuwa vikao vya Bunge hilo vinatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

"Subira yavuta kheri, tusubiri," amejibu Spika Ndugai.