Picha ya Gerd Muller enzi za uhai wake
Mshambuliaji huyo wa zamani ambaye alikuwa na jina la utani 'Der Bomber' alichukuliwa kama mmoja wa washambuliaji wakubwa kucheza mchezo wa soka na kuisaidia nchi yake kutwaa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 1974 na taji la Euro mwaka 1972.
Muller pia aliweka rekodi ya kua mfungaji wa muda wote wa Bayern Munich akiwa na mabao 552 katika mechi 607 alizocheza, huku akiwa na jumla ya magoli 711 katika michezo 780 kwa ujumla wake katika muda wake wote akicheza soka katika ngazi ya kilabu na timu ya taifa.