Tuesday , 17th Aug , 2021

Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya tatu Basil Pesambili Mramba, amefariki dunia asubuhi ya leo ya Agosti 17, 2021, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Regency Medical Center Jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 81.

Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya tatu Basil Pesambili Mramba, enzi za uhai wake

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, familia imeeleza kwamba kulingana na hali ya sasa ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 wanafamilia pekee ndiyo wanaoruhusiwa kufika nyumbani kwa marehemu Oysterbay.

Basil Mramba pia, aliwahi kuwa Mbunge wa Rombo mkoani Kilimanjaro, alizaliwa Mei 15, 1940.