Tuesday , 17th Aug , 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kumtafuta na kumkamata popote alipo mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, kwa kueneza uvumi kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

Kushoto ni Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima, na kulia ni Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima

Waziri Dkt.Gwajima, ametoa maagizo hayo wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Kyatungwe mkoani Mara.

Katika hatua nyingine Waziri Gwajima, amepiga marufuku watu wanaoeneza uvumi juu ya chanjo ya Corona ambapo amesema yeye ndio mwenye mamlaka ya kutangaza jambo juu ya afya.