Wednesday , 18th Aug , 2021

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) linasisitiza kuwa Kim Poulsen bado ni kocha mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars).

Kocha wa Taifa Stars,Kim Poulsen akiwa katika majukumu yake ya kazi

Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa TFF, inafanya mazungumzo na kocha Jamal Sellami kwaajili ya kuinoa Taifa Stars sio za kweli.

TFF inaendeshwa kiuweledi hivyo haiwezi kufanya maongezi na kocha mwingine wakati inamkataba na Kocha Poulsen.

Februari mwaka huu, TFF ilimteuwa Poulsen Kuwa Kocha wa timu ya Taifa Stars kwa mkataba wa Miaka Mitatu.