Monday , 23rd Aug , 2021

Mabingwa wa zamani wa VPL, Klabu ya Azam inataraji kuweka  kambi ya takribani wiki moja na nusu kwenye mji wa Ndola nchini Zambia ili kujiandaa na michezo wa mtoano ya hatua ya awali kuwania kufuzu kombe la Shirikisho barani Arika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Azam wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar kabla ya kukwea pipa kwenda nchini Zambia.

Azam ambayo imeondoka nchini Alfajiri ya leo Agosti 23 kuelekea Zambia, inataraji kucheza michezo mitano ya kirafiki na miamba ya Soka nchini humo ili kuwapa ushindani mzuri waoka mikate hao kutoka Chamazi ili ifanye vizuri zaidi kwenye michezo ijayo.

Michezo hiyo minne ya kirafiki ni dhidi ya Red Arrows ambayo ni timu ya Jeshi, mchezo utachezwa Agosti 25, Agosti 29 watamenyana na Zanaco huku mchezo watatu watakipiga dhidi ya Forest Rangers  mchezo utakaochezwa Septemba 2.

Michezo  mwingine ni ule watakaocheza dhidi ya Zesco United ambayo ni tumu ay Shirika la umeme nchini Zambia.

Na mara baada ya michezo hiyo, kikosi cha Azam kinataraji kjurejea nchini Septemba 5, 2021 tayari kwa mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Horseed ya Mogadishu nchini Somalia.

Michezo hiyo ya kirafiki inatazamwa kuwa sehemu kivutio cha mashabiki wa wanalamba lamba hao kwani wamewajumuisha wachezaji wao wapya waliowasajili kwenye kambi hiyo wakiwemo nyota watatu kutoka Zambia, Charles Zulu, Paul Katema, mshambuliaji Rodgers Kola, Mkenya Kenneth Muguna na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.