Sunday , 29th Aug , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania (TFS) kuyapiga mnada magogo ambayo yamevunwa kinyume cha utaratibu na watu wasiojuliakana kutoka katika Pori la Akiba la Igombe wilayani Kaliua mkoa wa Tabora.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja

Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya kufika na kuyaona magogo hayo katika katika  kijiji cha Wachawaseme wilayani Kaliua mkoa wa Tabora Agosti 28, 2021. 

Aidha Majaliwa amekagua mipaka ya Pori la Akiba la Igombe wilayani Kaliua, ambako aliagiza pori hilo lilindwe baada ya kushuhudia uharibifu unaofanywa na watu wanaokata miti, kuendesha shughuli za kilimo, uvuvi na makazi kinyume cha sheria.

Katika ukaguzi huo Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi. Dkt.  Batilda Burian.