
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula.
kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria.
Denmark ilitangaza uamuzi huo ambao ulihusishwa na mkakati wao mpya wa masuala ya mambo ya nje. Mbali na Tanzania pia nchi hiyo itafunga ubalozi wake nchini Argentina, Ubalozi mdogo wa Chongqing nchini China na ujumbe wa biashara huko Barcelona (Uhispania).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema hatua hiyo ya Denmark inasikitisha ikizingatiwa kuwa hivi karibuni Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikifanya jitihada za kufufua na kuimarisha diplomasia na uhusiano wa nchi rafiki ikiwemo Denmark.
Aidha taarifa hiyo inaeleza Balozi Mulamula alifanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark, Flemming Mortensen ambapo walikubaliana kuendelea kushirikiana na Mortensen anatarajia kuzulu nchini siku zijazo.
“Pamoja na hatua iliyochukuliwa na Denmark, ni matarajio ya Tanzania kuwa Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono ajenda za Tanzania katika Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na majukwaa mengine ya kimataifa,” inaeleza taarifa hiyo.
Baada ya kuwapo kwa takribani miongo sita, Denmark imetangaza kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024, huku sababu zikitajwa kuwa ni kuendana na mpango wa nchi hiyo katika masuala ya kimataifa. Uamuzi huo ulitangazwa Agosti 27, 2021 na Waziri wa Mambo ya nje wa Denmark, Jeppe Kofod.