
Lionel Messi akionekana kwenye matukio tofauti tofauti likiwemo tukio la kumuonesha akiwa anajiandaa kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Neymar dakika ya 66 kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na PSG, PSG iliposhinda kwa mabao 2-0 yote yakifungwa na Kylian Mbappe.
6 - Ni idadi ya miaka iliyopita tokea Max Verstappen raia wa Ubelgiji aweke rekodi ya kuwa dereva mwenye umri mdogo zaidi, miaka 17 na siku 166 kushiriki kwenye mashindano ya mbio za magari ya Australian Grand Prix.
Mkali huyo wa kupiga gia, ameibuka kuwa mshindi wa mashindano ya Belgium Grand Prix baada ya mashindano hayo kulazimika kuhairishwa kwenye mzunguko wa pili tu kufuatia mvua kali zilizopelekea uono hafifu kwa madereva na kumpa faida ya kikanuni Verstappen kutoka timu ya Red Bull kuwa mshindi na kuwapiku George Russell kutoka timu ya Williams na Lewis Hamilton kutoka Mercedes.
Wakali hao watachuana tena wikiendi ijayo kwenye mashindano ya Dutch Grand Prix.
5 - Ni wastani wa Assist alizopiga mlinzi mkongwe Rajon Rondo mwenye miaka 35 na points 8 alipokuwa na timu ya Los Angeles Clippers msimu uliopita kabla ya Clippers kumuacha ajiunge na Memphis Glizzles kwenye sehemu ya dili ya mabadilishano ya mchezaji Erick Bledsoe kutoka Memphis kwenda Clippers Agosti 15 mwaka huu.
Mchezaji huyo inaelezwa yupo tayari kununua mkataba wake ili awe mchezaji huru wakati amabo timu yake ya zamani ya Los Angeles Lakers ikielezwa kuwa mstari wa mbele kutaka kumsajili baada ya kuishi na mchezaji huyo kwa miaka 2 tokea 2018 hadi 2021 na kuwa sehemu ya msaada kwa Lakers kubeba ubingwa wa NBA.
Usajili wa Rondo endapo ukikamilika basi ataungana na wakali wengine kama Russell Westbrook almaarufu 'Triple double machine' na 'Carmelo Anthony ambao tayari walijiunga na Lakers mwezi uliopita.
4 - Ni idadi ya mabao yaliyofungwa kwenye michezo yote mitatu ya EPL iliyochezwa jumapili ya jana Agosti 29, 2021 ambapo Burnley 1-1 Leeds Utd, Spurs 1-0 Watford na kuongoza ligi wakina na alama 9 ushindi wa 100% kwenye michezo 3 wakati Man Utd wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wolves na kushika nafasi ya 3 wakiwa na alama 7.
Bao la Spurs limefungwa na Son Hueng-Min aliyekuwa anafikisha mchezo wake wa 200 kwenye EPL na bao lake la 3 msimu huu Ilhali bao la Man Utd limefungwa na Mason Greenwood ambaye pia amefikisha bao lake la 3 msimu huu kwenye EPL.
Ushindi wa Man Utd wamewafanya waweke rekodi ya kibabe ya kuwa timu pekee kucheza michezo mingi bila kufungwa wakiwa viwanja vya ugenini, michezo 28 ' Ole Gunnar Solskjaer at the Wheel'.
3 - Ni idadi ya misimu ambayo klabu ya Yanga imefanikiwa kufanya tamasha lake la yanga day lijulikanalo 'Siku ya Wanachi' tokea mwaka 2019 na msimu wa tatu kukamilika baada ya kulifanya Jumapili ya Jana Agosti 29 kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es salaam.
Tamasha hili lilianza na michezo miwili ya utangulizi, Yanga U20 walitolewa ushamba baada ya kufungwa 3-1 na Cambiaso Academy FC wakati Yanga Princess walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Ilala Queens.
Aliyekuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mh. Hemed Suleiman Abdulla kabla ya kubariki mchezo wa kirafiki mahsusi wa kutamatisha tamasha hilo, aliwasihi viongozi na mashabiki wa Yanga kumaliza makando kando, wawe wamoja kwani anaamini Yanga itakuwa mabingwa kutokana na usajili walioufanya.
Baada ya kusema hayo tamasha hilo lilitamatishwa na mchezo wa kirafiki ambapo Yanga walifungwwa 2-1 na Zanaco ya Zambia huku kipa wa Yanga, Djigui Diarra aliyepambwa kuwa na uhodari wa kudaka hadi mishale lakini alishindwa kudaka shuti kali la nje ya 18 la Kelvin Kapumbu dakika ya 76 lililoipa Zanaco Ushindi huo na kutibua sherehe yenyewe.
2 - Ni idadi ya magoli alitofunga Kylian Mbappe na kuipa ushindi PSG wa mabao 2-0 dhidi ya Reims na kuongoza ligi kuu ya Ufaransa wakiwa na alama 12 baada ya ushindi wa michezo yote 4.
Mchezo huo uliambatana na tukio lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa PSG la kumuona Messi akiichezea mchezo wake wa kwanza na hatimaye tukio hilo likatimia baada ya Lionel Messi kuingia dk66 kuchukua nafasi ya Neymar na kumfanya Messi acheze mchezo wake wa kwanza akiwa na PSG lakini ni wa kwanza tokea Julai 10 alipocheza fainali ya COPA AMERICA na kutwaa ubingwa huo mbele ya Brazil.
1 - Ni nafasi anayoshikilia Novak Djokovic kwenye viwango vya ubora vya tennisi duniani kwa wanaume baada ya kuwa kwenye kiwango bora kwa kushinda Grand Slam tatu yaani Australian Open, French Open & Wimbledon zote ndani ya mwaka 2021.
Jina la nyota huyo ni miongoni mwa majina maarufu kabisa yaliyosalia kwenye michuano ya US Open inayotari kuanza baadae ya leo na kama Djokovic atafanikiwa kuwa bingwa wa michuano hiyo basi ataweka rekodi ya kuwa mcheza tennis wa kwanza kushinda grand slam 4 ndani ya mwaka mmoja tokea Rodney Laver afanye hvyo mwaka 1969.