
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe
Hilo limeelezwa leo kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Elinaza Luvanda.
Katika kesi hiyo upande wa washtakiwa ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala uliibua hoja ya kutaka kesi hiyo ifutwe kutokana na Mahakama ya Mafisadi kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za Ugaidi.
Aidha kwa upande wa Jamhuri ulipinga hoja hiyo na kusema Mahakama hiyo ina mamlaka.