Wednesday , 1st Sep , 2021

Nahodha msaidizi wa kikosi cha Taifa Stars, John Bocco, hajajumuishwa katika kikosi cha Kocha Kim Poulsen kitakachoikabili DR Congo katika mechi ya kundi J ya  kufuzu Fainali ya Kombe la Dunia itakayochezwa kesho katika Jiji la Lubumbashi.

Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Rafael Bocco.

Wachezaji wengine walioachwa kwenye orodha ya majina 23 ni pamoja na Zawadi  Mauya,Ramadhani Kabwili,Kennedy Juma na Edward Manyama.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa kwanza kusaka tiketi ya kufuzu mashindano ya kombe la dunia siku ya kesho dhidi ya DRC Congo katika dimba la Stade TP Mazembe , Lubumbashi.

Ikumbukwe kuwa Stars ilifuzu hatua ya pili ya mashindano haya baada ya kuifunga timu ya taifa ya Burundi na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi, huku Tanzania ikipangwa kundi J, na DRC Congo, Madagascar na Benin.

Orodha ya kikosi kamili kilichowasili nchini DRC Congo kwaajili ya mchezo wa kesho ni:

Makipa: Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata, Wilbol Maseke (Azam).

Mabeki: Shomari Kapombe (Simba), Israel Mwenda (Simba), Erasto Nyoni (Simba), Dickson Job (Yanga) and Bakari Mwamnyeto (Yanga) , Lusajo Mwaikenda (Azam), Abdulrazack Mohamed (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Nickson Kibabage (Youssofia FC - Morocco).

Viungo: Meshack Mwamita (Gwambina) and Novatus Dismas (Maccabi Tel Aviv – Israel). Mzamiru Yassin (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Feisal Salum (Yanga), Salum Abubakar (Azam).

Washambuaji: Iddy Selemani (Azam), Abdul Suleiman (Coastal Union),Ayoub Lyanga (Azam) Mbwana Samatta (Fenerbahce - Turkey),and Simon Msuva (Wydad Casablanca - Morocco).